Sunday , 8th Jun , 2014

Muigizaji maarufu wa vichekesho nchini Tanzania Saidi Ngamba maarufu kama Mzee Small amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya taifa Muhimbili alikokimbizwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Mzee Small akiwa na Bi. Chau

Taarifa za kifo cha Mzee Small zimethibitishwa na mtoto wake wa kiume ambaye amesema baba yake amefariki kutokana na kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kiharusi.

Mtangazaji wa Radio One Bibi Chausiku Salum maarufu kama Bi. Chau ambaye amewahi kuigiza na Mzee Small amezungumzia kifo hicho na kueleza kuwa kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya uigizaji.

Bi. Chau amekitaja kifo cha Mzee Small kama hazina iliyopotea kutokana na kuwa na uzoefu mkubwa katika masuala ya sanaa ya uigizaji.