Monday , 2nd Jun , 2014

Mwili muongozaji filamu maarufu nchini Tanzania Marehemu George Tyson, utaagwa keshokutwa Jumatano saa 4 asubuhi katika viwanja vya Leader Club Kinondoni jijini Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao nchini Kenya kwa Maziko.

mtayarishaji wa filamu George Tyson

Taarifa hizi ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere ambapo hii itakuwa ni nafasi maalum kwa wadau, mashabiki na wote wanaoguswa na msiba huu mkubwa kutoka hapa Tanzania, kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Tyson.

George Tyson anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu na utayarishaji vipindi vya televisheni, ambapo kati ya kazi zake mbalimbali, alikuwa ni mtayarishaji ya kipindi cha The Mboni Show kinachorushwa hapa na EATV.

eNewz tunaitakia roho ya Marehemu mapumziko mema mahala pema peponi Aamin.