
Ibra Nation amebainisha hayo alipokuwa anazungumza na PLANET BONGO ya East Africa Radio hii leo, na kusema kwamba haoni haja ya kutengeneza kiki mitandaoni kwa kuwa muziki wake umejitosheleza kwa kila jambo na ndio maana ameweza kushilika soko kwa upande wake.
"Muziki ambao ninaoufanya mimi hauwitaji kiki wala kitu chochote kile, watu wanakubali muziki wangu kwa jinsi ulivyo. Watu wanapenda ujumbe ninaoipamba ambao unaponya nafsi zao 'sometimes' hata mahusiano yao. Nimeshapata 'comment' hizo kibao kwa watu, kuwa walikuwa wamezinguana lakini baada ya kusikia nyimbo zangu wameweza kurudi na kuwa pamoja", amesema Ibra Nation.
Ibra Nation.
Ibra Nation ni miongoni mwa wasanii wachanga walioweza kuteka hisia za watu wengi kupitia wimbo wake wa 'nilipize' aliutoa mwaka 2017 na kujigamba sehemu mbalimbali kuwa yeye ndio msanii pekee ambaye anaweza kumshusha Aslay kutumia ala za sauti yake.
Msikilize hapa chini Ibra Nation anavyofunguka zaidi..