Thursday , 3rd Dec , 2015

Aliyekuwa Mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki wa dansi nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ amefariki dunia.

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini kutoka Kongo, marehemu Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’

Kwa mujibu wa wanamuziki waliofanya naye kazi kwa muda mrefu, Kasongo amefariki dunia nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar es salaam siku ya jana, baada ya kuumwa kwa muda mrefu akisumbuliwa na kisukari, hivyo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake.

Marehemu katika enzi ya uhai wake alifanya kazi na bendi kama Maquis du Ziare, ambapo siku za mwisho za uhai wake aliitumikia Bendi ya Bakulutu kabla ya kujiunga katika Bendi ya Bana Maquis.

eNewz tunatoa pole kwa wote wanaoguswa na msiba huo, na kuitakia roho ya marehemu mapumziko mema mahala pema peponi, Amin.