Thursday , 16th Jul , 2015

Nyota wa miondoko ya afro-Pop wa nchini Burundi Kidum, amesikitishwa sana na kifo cha mchekeshaji nyota wa nchini humo mzee Ojwang' kutokana na kwamba alimuhitaji mkongwe huyo kuigiza katika video ya wimbo wake 'Mulika Mwizi'.

Nyota wa miondoko ya afro-Pop wa nchini Burundi Kidum

Kidum ambaye mwenye makazi yake nchini Kenya ameongea na eNewz akiwa jijini Nairobi amesema kuwa alikuwa akijitahidi kumtafuta marehemu Ojwang' kwa ajili ya project ya kuigiza kwenye kichupa cha wimbo huo, lakini gwiji huyo alikuwa bize akifanya kazi katika kipindi cha televisheni nchini humo.

Ila pamoja na yote Kidum amemwagia sana sifa marehemu Ojwang' kwa kipaji chake kikubwa katika ulimwengu wa burudani kwani Kenya ina kila sababu ya kujivunia kazi za gwiji na mkongwe huyo aliyeitangaza nchi hiyo kimataifa kupitia katika sekta ya burudani nchini humo.