Wednesday , 7th May , 2014

Rapa wa nchini Kenya Nonini ambaye pia ni baba wa mtoto wa kiume mwenye miaka miwili sasa, ameweka wazi kuwa mtoto huyu ambaye anafahamika kwa jina Jaden, amembadilisha sana maisha yake, mtazamo wake wa maisha na vile vile muziki ambao anaufanya.

Jay na Nonini

Nonini ameweka wazi kuwa, mtoto huyu kutokana na kuonyesha tabia ya kuiga kila kitu anachokifanya, amemsababisha kuwa na huzuni kwa kuogopa kukosea kitu na hivyo kuwa mfano mbaya kwa mtoto huyu ambaye anataka malezi yake yawe ya aina yake kuhakikisha kuwa anakua mtu bora.

Rapa huyu akiwa kama baba amesema kuwa, kutoka kwa mtoto wake huyu, kinachomshangaza na kumfurahisha zaidi pia ni uwezo wake wa kuiga nyimbo zake na hata kile anachokifanya katika video za muziki wake, kitu kinachoashiria kuwa huenda mtoto huyu akaja kuwa mkali zaidi katika fani ya baba yake.

Tags: