Saturday , 31st Jan , 2015

Msanii wa muziki Peter Msechu amesema kuwa, baada ya ngoma yake ya Nyota kufanya vizuri nnje ya mipaka ya nchi hususan huko Nigeria amegundua kuwa melody,ubora na mpangilio wa vyombo mara nyingi ndio kitu pekee ambacho huvuta watu kupenda wimbo.

Peter Msechu

Amesema watu wanapenda melody na si ujumbe uliopo ndani yake na kuwezesha rekodi husika kufanya vizuri hata nje ya mipaka.

Msechu amesema kuwa, kuna haja ya wasanii wa hapa nyumbani kushikilia misingi ya muziki wa hapa nyumbani na kuzingatia vitu hivi huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kuvuka mipaka endapo rekodi ambayo mtu atafanya itakuwa na ubora na midundo na melody ya kuvutia.