Saturday , 8th Mar , 2014

Msanii wa muziki mwenye mafanikio makubwa kutoka nchini Kenya, Jaguar amekuwa na kila sababu ya kufurahia matunda ya misaada ambayo amekuwa akitoa kwa jamii, kubwa zaidi kwa sasa likiwa ni kufaulu kwa mwanafunzi

Hii ni kutoka katika matokeo yaliyotoka hivi karibuni kwa ngazi ya cheti cha elimu ya sekondari huko Kenya, ambapo mwanafunzi huyu amefanikiwa kupata daraja la kwanza.

Hatua hii ya mafanikio ambayo imempatia moyo zaidi Jaguar ambaye ni mfadhili wa Rensom, na kupitia ukurasa wa instagram wa msanii huyu ameweka picha yake akiwa pamoja na mwanafunzi huyu ambapo amemuahidi kuendelea kumsaidia zaidi kumfikisha katika ndoto zake za kuwa Injinia mwenye vyeti vya juu kabisa.