Tuesday , 30th Sep , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Kenya, Colonel Moustapha ameamua kuonyesha mfano mzuri kwa jamii kwa kujiunga na chuo cha Mt Kenya huko Thika kwaajili ya kujiendeleza kimasomo.

msanii wa muziki nchini Kenya Colonel Moustapha

Msanii huyu ambaye amekuwa akisongwa na sifa mbaya mara nyingi, safari hii ameamua kuwa kioo cha jamii ambapo malengo yake ni kujipatia shahada ya Usimamizi wa Biashara pale atakapohitimu.

Colonel Moustapha amesema kuwa, ameamua kuchukua hatua ya kurudi shule ili kuipeleka juu zaidi fani yake.