Kikosi cha kwanza ambacho kitalichakaza jukwaa ni pamoja na mkali wako Ommy Dimpoz, Kala Jeremiah, Ben Pol, Ney Wa Mitego, Mwana FA, Khadija Kopa, Warriors from The East, Young Killer, Proffesor jay, Jambo Squad na Weusi.
Burudani yote hii ni ya mapema, ambapo milango itafunguliwa saa nne asubuhi hadi saa 12 jioni kwa kiingilio cha shilingi 2500 tu, ambapo pia utapatiwa Bia yako ya Kilimanjaro Bure.
Moshi eeh tukutane kesho pale uwanja wa Ushirika Moshi kwenye Kilimanjaro Music Tour 2014, halafu Tuzungushe Kikwetu kwetu.