Wednesday , 13th Jan , 2016

Nyota wa muziki Cynthia Morgan amezungumzia ugomvi wake na msanii wa muziki Davido ambaye amemtuhumu kwa kumuita majina ya kejeli katika mtandao unaosambaa kwa kasi sasa wa Snapchat, kitu ambacho binafsi hakukipenda na kujibu mashambulizi.

Nyota wa muziki Cynthia Morgan wa nchini Nigeria

Morgan ameingia ndani zaidi na kueleza kuwa, Davido alianzisha ugomvi wao huo kwa kumuita n'gombe, hatua ambayo imemfanya mwanadada huyo kumuwakia Davido na lebo yake nzima ya HKN, akikazia kuwa hana kinyongo chochote na mahasimu wake hao baada ya kujibu mashambulizi.

Mwanadada huyo pia ametumia nafasi hiyo kukanusha uvumi kuwa ana hisia za kimapenzi kwa Davido, akionesha kushangazwa na chanzo cha uvumi huo ingawa anakiri kuwa anapenda sana kazi za msanii huyo anayefanya vizuri Afrika.