Saturday , 10th Jan , 2015

Muigizaji wa filamu hapa Bongo, Yvone Cherry maarufu kama Monalisa, amesema kuwa milango ya kufanya kazi za filamu kimataifa imeanza kufunguka, akiwa tayari na project aliyofanya na timu kutoka Marekani, Daddy's Wedding itakayotoka Februari 14.

Monalisa

Monalisa amesema kuwa, mbali na kazi hii, ana project nyingine na timu kutoka UK kati ya nyingine ambazo zinaonesha kuwa taratibu sanaa hii imeanza kuvuka mipaka kuelekea kule kunakotakikana,.

Vilevile Star huyu wa filamu akaelezea matamanio yake ya kuona siku moja soko la filamu Afrika linaungana na kuwa kitu kimoja, na wasanii wote wa bara hili kuungana na kufanya kazi kwa ushirikiano.