Friday , 25th Jan , 2019

Baada ya muigizaji Kajala Masanja kuwa kimya baada ya matokeo ya kidato cha nne, uvumilivu umewashinda mashabiki pamoja na wafuasi wa mitandao ya kijamii wakimtaka muigizaji huyo kuweka wazi matokeo ya mtoto wake Paula aliyemaliza kidato cha nne mwaka 2018.

Kushoto ni muigizaji Monalisa, Mtoto wa Kajala (Paula) kulia

Gumzo hilo la mashabiki limezidi hasa katika mtandao wa Instagram baada ya Muigizaji Monalisa kuelezea furaha yake baada ya binti yake (Sonia) aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana kufaulu kwa kupata alama A katika mosomo yake yote 7.

Monalisa aliandika, "Machozi yananimwagika. Nakosa cha kusema. Ahsante mwanangu. Divisio One? Na 'A' ya Maths? Uwiiii, nakupenda mwanangu".

Kwa upande mtoto wa Kajala (Paula) ambaye tayari ni maarufu amezua minong'ono miongoni mwa watu kwa ukimya wa matokeo yake ambapo watu wamekuwa wakiulizana huku wengine wakimtetea binti huyo ambaye bado matokeo yake hayajajulikana.

binti_michambo :  Jamani kwani kuna habari gani?? #Paula Kapata Division Ngapi tumpongeze Kajala ebu tupe 'info' kukaa kimya huko Veeepe?.

yaliyomoyamo: Kajala mbona hutuambii matokeo ya binti yetu #Paula umetufanya adi wambea tunateseka kufyekenyua huku na kule. Ila Paula umejua kumfedhehesha mama ako  four ya 32 kweli?.

udaku_dsm : kajala kama matokeo ya mtoto huja ya 'publish' ikiwa kwenye mahafari ya from four ya mwanao ulisumbua Instagram nzima halafu hautupi feedback za mtoto wako, Basi sio mbaya kila la kheri mi namuombea hata awe video queen.

surazamastaa : Paula Kapata Division Ngapi? tumpongeze Kajala ebu tupe taarifa kama ulivyotupa za graduation kukaa kimya huko Veeepe?.

the_originaleast: Acheni hizo bwana. Mnauliza matokeo kama mlisadia kulipa 'school fees' kila mtu anakitu alichoandikiwa kwenye safari yake ya Maisha. Wangapi walipata Div 1 form 4 , one form six na wamemaliza chuo bado wanasota  na wangapi form four walipata zero but wametuacha kimaisha!. Acheni kufanya hivyo . Mnaona raha kupost but mnasahau yule ni mtoto !!! Social media kum-bully kuhusu matokeo hachelewi kujidhuru!. Ni matokeo tu sio mwisho wa maisha.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk. Charles Msonde, matokeo yaliyotangazwa siku ya jana yanaonyesha kuongezeka kwa ufaulu kwa watahiniwa kwa asilimia 1.28 kutoka asilimia 77.09 ya mwaka 2017 hadi asilimia 78.38 mwaka 2018.