Monday , 1st Dec , 2014

Rapa Khaligraph kutoka nchini Kenya, ameachia rekodi ya ngoma inayokwenda kwa jina 'Hands In The Air', kazi ambayo ndani yake amemshirikisha dada yake ambaye anafahamika kwa jina Totti.

msanii wa nchini Kenya Khaligraph

Rapa huyu ametoa shavu hili kwa dada yake huyu katika kibwagizo cha rekodi hii ya kujirusha, akiwa pia ndani yake amemshirikisha Frobbo kutoka Swagcitty Records.

Khaligraph ameendelea kudhihirisha uwezo mkubwa katika gemu ya michano, akiwa tayari na kazi hii mpya iliyotoka katika kipindi ambacho video ya ngoma yake ya 'MBesha' bado inafanya vizuri katika chati mbalimbali za muziki.