Saturday , 14th Jun , 2014

Rapa Mike Tee ameweka wazi mpango wake wa kusaidia wasanii kupata uwanja mkubwa zaidi wa playtime ya rekodi zao.

Mike Tee

Maamuzi haya ni kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa wasanii na kazi zao kila siku, huku "Media" na muda wa kazi hizi kuchezwa hewani ukiwa mdogo.

Mike Tee ameieleza eNewz kuwa, ameibuka na mpango huu ambao ameupatia jina Kitaa baada ya utafiti wa miaka kadhaa, ambapo yeye binafsi katika hatua hii ya awali atakuwa akisambaza kazi za wasanii ambao amekubaliana nao kwa madereva mabajaji na pikipiki ambao wamekuwa ni njia nyingine nzuri ya kuzifanya kazi zawasanii kusikika katika kona za mitaa.

Mike Tee ambaye kwa sasa amerejea katika chati na ngoma mpya inayokwenda kwa jina Mchepuko, anafunguka hapa kuhusiana na Project Kitaa.

Tags: