Thursday , 8th Jan , 2015

Msanii wa Bongo Fleva nchini Mike Tee ametolea ufafanuzi kutokana na kuyumba kwa baadhi ya wasanii katika game ya muziki na wengineo kushindwa kuendelea kushikilia nafasi ya juu katika sanaa hiyo kwa muda mrefu.

Msanii wa Bongo Flava nchini Mike Tee

Mike Tee amesema kuwa hiyo ni hali ya kawaida katika muziki kama ambavyo ipo kwa biashara nyingine zozote zile.

Aidha msanii huyo amesema kuwa, changamoto inayowasumbua wasanii wengi ni kukosa 'Plan B' pale muziki unapotetereka na kushindwa kuhimili ushindani na mabadiliko katika muziki, na hapa staa huyu ambaye alikwishawahi kuzikamata vilivyo chati za muziki hapa bongo anaeleza.