Tuesday , 20th Sep , 2016

Mdau wa muziki nchini Fredrick Bundala, amewataka wasanii kwenda kuchukua fomu za kushiriki EATV AWARDS, kwani ni jambo la msingi kwa kila msanii kushiriki huku akiwaondoa hofu kuhusu mfumo mpya wa kujisajili katika tuzo hizo.

Fredrick Bundala

Akizungumza na East Africa Television, Bundala amesema ingawa utaratibu uliowekwa wa kujisajili ni mgeni kwa wasanii, lakini ni mfumo mzuri kwani unaweka uwazi, hivyo ni wakati sasa wasanii wafahamu wajibu wao na kuacha kujikweza kwa umaarufu walionao na kwenda kujaza fomu za kujisajili kushiriki EATV AWARDS .

"Ingawa ni kitu kigeni kidogo kwao unajua, sio tuzo zote zinakuwa na uwazi kama hivi, ukiangalia hapo msanii anajipendekeza mwenyewe, kwa hiyo kila kitu kinawekwa 'open', kwa hiyo msanii asione ni kujishusha, au akaona mimi ni msanii mkubwa nitajazaje fomu, wasanii wachukue fomu waweke eagle pembeni", alisema Fredrik Bundala ambaye ni moja ya watu ambao wako karibu sana na wasanii na mwenye mchango kwa tasnia ya sanaa nchi.

EATV AWARDS zimeweka mfumo huo wa msanii pamoja na kazi yake kujisajili, ili msanii akubali mwenyewe kuwa anataka kushiriki kwenye tuzo hizo na kukubaliana na vigezo na msharti yake, tofauti na baadhi ya tuzo zilizozoeleka.

Tags: