Thursday , 16th Apr , 2015

Makala ya filamu inayohusu mauaji ya Kimbari yaliyotokea mnamo mwaka 1994 nchini Rwanda inatarajiwa kutoka hivi karibuni huku muongozaji na muigizaji Liane Muhoza Muta-ganzwa akitarajiwa kuweka matokeo halisi ya vita hivyo.

muigizaji na muongozaji Liane Muhoza Mutaganzwa wa Rwanda

Liane Muhoza ambaye naye alipoteza watu wake wa karibu katika mauaji hayo ameelezea kuwa makala hiyo yaani Documentary ambayo imeanza kufanyiwa upigaji picha, inaelezea maisha ya Muhoza baada ya mauaji ya halaiki na jinsi alivyoweza kusambaza ujumbe wa kuleta umoja nchini humo.

Hii itakuwa ni moja ya makala kubwa ambayo itaanza kuoneshwa ndani ya wiki hii ambayo imemwacha mwanadada huyo yatima baada ya baba yake kuuawa ambapo pia itahusisha watu walionusurika katika mauaji hayo ambayo wameanza maisha mapya baada ya kupitia mauaji hayo makubwa kuwahi kutokea nchini humo.