Wednesday , 14th Jan , 2015

Wasanii wa muziki kutoka orodha iliyosheheni wakali watakaofanya onesho kali katika tamasha la tiGO Kiboko Yao tarehe 24 mwezi huu Leaders Club Jijini Dar es Salaam, wameonesha utayari wa kutoa burudani siku ya onesho.

Mwimbaji wa miondoko ya taarabu nchini Isha MAshauzi

Katika mahojiano binafsi na eNewz, msanii wa muziki Christian Bella, Isha Mashauzi kati ya wengine kibao, wamewataka mashabiki wao kukaa tayari kwa kushuhudia nguvu na upya wa burudani, katika tamasha hilo lenye hadhi ya kimataifa la tiGO Kiboko Yao ikiwa ni onesho lao kubwa kabisa la kuanzia mwaka.