Tuesday , 12th Jan , 2016

Sherehe za kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanyika leo Tanzania Visiwani na kudhuriwa na viongozi mbalimbali, huku kukiwa na hisia tofauti kutoka kwa wananchi wa visiwani humo kuhusiana na tukio hilo la kihistoria.

msanii wa miondoko ya mduara kutoka Zanzibar AT

eNewz leo hii tumeongea na msanii kutoka Zanzibar, Baby J ambaye amesema kuwa katika kudhihirisha na kuunga mkono sherehe hizo, wakishirikiana na wasanii wengine wa Zanzibar, wamepanga kukutana kesho na kutembelea kaburi la muasisi wa mapinduzi hayo, Marehemu Karume wakiwakilisha kundi kubwa la wana mapinduzi kutoka Bara na Visiwani.

Lakini kwa upande wa pili AT, akiwa pia anawakilisha kundi kubwa la wazanzibari nyuma yake, ameeleza kuwa hana imani na suala zima la Mapinduzi akiona linapoteza maana yake, akitaka utulivu kwa Wazanzibari na Serikali kuchukua hatua kurejea uchaguzi kwa haki kurudisha imani ya wananchi wake.