Wednesday , 29th Apr , 2015

Msanii wa muziki Malfred ambaye ameachia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la Kwanini, amesema kuwa bado kuna uzito mkubwa wa mashabiki kutoka hapa nyumbani kuwasapoti wasanii wao, ukilinganisha na nje ya nchi.

msanii wa bongofleva nchini Malfred

Malfred amesema kuwa, kwa uzoefu wake nje ya nchi licha ya mashabiki kutokuelewa kiswahili, mapenzi wanayo muonesha humfanya atamani kulia, na hii ndiyo tofauti kubwa ya mashabiki kutoka hapa Tanzania na wale Malfred anaokutana nao nje ya nchi.