
Rapa One the Incredible akiwa Nikki Mbishi, upande wa kushoto huku Producer Abbah Process akiwa kulia.
Hayo yamebainishwa na rapa mkongwe Nikki Mbishi, One the Incredible pamoja na 'producer', Abbah Process walipokuwa wanazungumza na eNewz inayorushwa na EATV baada ya kuwepo makundi mengi ya wasanii, ambayo kwa namna moja ama nyingine yamekuwa yakionekana kuua muziki nchini, kwa kile kinachodaiwa ubinafsi baina ya kundi na kundi na kupelekea wasanii wengine kushindwa kupata nafasi ya kupata 'collabo'.
"Umoja wa wasanii umebakia kwenye matatizo tunayopata kama vile msiba ndio utaona watu wanakusanyika pamoja lakini katika vitu vingine hakuna umoja kabisa kutoka na makundi yaliyokuwepo", amesema Nikki Mbishi.
Naye, rapa One the Incredible amedai endapo hakutokuwa na maslahi yanayopatikana kupitia umoja basi ni ngumu kuona watu wakiwa wamejiweka wote katika eneo hilo.
"Hakuna kundi la watu ambalo linaloishi maisha tofauti kabisa ya kidunia ambalo linaweza kukubalia katika suala moja kama haliwanufaishi wote, kwa hiyo tukizungumzia suala la umoja katika sehemu zote huwa unakuja pale mnapokubaliana kwamba kila mmoja wapo anacho kitu anachonufaika nacho. Hapo ndipo umoja utakuwepo lakini hayo mengine yote ni maneno tu", amesisitiza One the Incredible.
Kwa upande wake, Producer Abbah Process amekuwa na mtazamo tofauti na wenzake kwa kile alichokidai, kuwa hakuna sababu ya wasanii kutengana kwa sababu wote wanafanya kazi ya aina moja hivyo ni muhimu kushirikiana kama ndugu ili kuweza kuufikisha mbali muziki wa Tanzania.