Monday , 10th Aug , 2015

Nyota wa muziki wanaoiendesha Afrika, Mafikizolo kutoka Afrika Kusini, Sauti Sol kutoka Kenya na Ali Kiba kutoka Tanzania kati ya wengine wanatarajiwa kuandika historia mpya kwa upande wa tasnia ya burudani hapa Bongo.

Onyesho kubwa la muziki la Party in The Park litakalofanyika jumamosi hii jijini Dar es Salaam

Onyesho hilo kubwa kabisa la kukata na shoka litakalofanyika Jumamosi hii Jijini Dar es Saalam limepewa jina la Party in The Park, na litafanyika The Green Oysterbay Kenyatta Drive Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 6 mchana mpaka saa 1 Jioni.

Ukiwahi kununua tiketi yako mapema sasa unaweza kuipata kwa bei ya kawaida ya shilingi 25,000 ama shilingi 30,000 getini siku ya tukio, na VIP kwa sasa tiketi inauzwa kwa shilingi 60,000 ama 100,000 getini siku ya tukio.

Unaweza kujipatia tiketi yako mapema katika maeneo yafuatayo: Eaters point Namanga, Eater's Point Oysterbay, TiME Tickets, tiketi.co.tz ilovedar.com, Rainbow Social Club, George & Dragon -Tanzania Break Point Kinondoni, KCB Mlimani City, KCB Kariakoo, KCB Samora Avenue, Catalunya Pub Sinza na Shangrila Oysterbay.

Onyesho hili linadhaminiwa na EATV na East Africa Radio.