Madee
Msanii aliyeiponda ni Nay wa Mitego aliiponda aliyesema kuwa si kazi nzuri kutokana na uandishi wa Madee na kusema ni ngoma nyepesi japo yeye alipenda zaidi mdundo wake.
Kwa nyakati tofauti wakongwe hao wameonesha kufurahishwa na ngoma hiyo na kusema hizo ndizo kati ya kazi ambazo zinatakiwa sasa kwa wananchi, kazi ambazo zinafanya watu wafurahie muziki mzuri.
"Mimi nimependa sana hii ngoma, Madee madude kama haya ndiyo yanatakiwa kusikika mitaani babu, aminia" alisikika Fid Q akisifia kazi hiyo ya Madee
Kwa upande wake Mwana FA pia aliipa shavu ngoma hii ya Madee ambaye amesema kuwa hiyo ni moja ya kazi nzuri na kwamba yeye hana tatizo nayo kwa kuwa ni kazi nzuri.
Lakini pia Madee aliamua kumpa majibu Mwana FA aliyehoji kwa utani kuwa ni kwanini kwenye ngoma hiyo Madee alisema "Manzese Music baby..."? Haya ndiyo yalikuwa majibu ya Madee
"Mwana FA siku hizi Manzese hakuna tena wasela Khamis, wamebaki wachache sana ambao nadhani mwakani hawatakuwepo kabisa sababu tunazificha hela hivyo watakaa na njaa watarudi kwao sababu ni wageni pale" aliandika Madee