Saturday , 11th Oct , 2014

Kufuatia kutangazwa kwa takwimu kuwa watanzania zaidi ya 2000 wapo katika Magerezani mbalimbali nchini wakikabiliwa na adhabu ya kifo, Rapa Madee kutoka Tip Top Manzese ametoa maoni yake kuwa adhabu hii sio sawa kabisa.

Madee

Madee ambaye amepitia mapicha mengi katika maisha yake kabla ya muziki kumuweka katika ramani nzuri, amesema kuwa, kila binadamu anastahili nafasi ya pili katika maisha yake na angependa siku moja kusikia adhabu hii imeondoshwa duniani.