Tuesday , 9th Sep , 2014

Wasanii wa muziki wa kundi la Mabaga Fresh, wakitamba na ngoma yao iitwayo 'Usimpe Pombe', wameweka wazi kuwa, ukimya wao wa muda ulikuwa ni kwa ajili ya kujipanga upya hasa baada ya kushuhudia mabadiliko makubwa katika soko la muziki.

kundi la muziki nchini Tanzania la Mabaga Fresh

DJ Snox kutoka katika kundi hili ameiambia eNewz kuwa, kwa sasa wameamua kurejea na kazi mpya ambayo ipo katika mtindo wa kisasa wa muziki, kazi ambayo wapo katika mchakato wa kuiandaa video yake.

Kwa upande wa JB, mkali huyu kutoka Mabaga Fresh amesema kuwa ujio huu ni wa tofauti na wa kishindo, huku akiahidi mashabiki mambo makubwa.