Thursday , 24th Apr , 2014

Nyota wa filamu wa kimataifa mwenye asili ya Kenya, Lupita Nyong'o anatarajia kutangaza uhusika wake katika filamu nyingine kubwa hivi karibuni, akiwa na changamoto ya kukidhi matarajio ya mashabiki na wadau wa filamu.

Lupita Nyong'o

Kumekuwa na tetesi mbalimbali kuhusiana na filamu itakayofuata kutoka kwa mwanadada huyu huku “Star Wars: Episode VII” na “Americanah.” zikitajwa katika orodha ya kazi anazotarajiwa kushiriki, ingawa wakala wa mwanadada huyu hakuthibitisha taarifa hizi na kusema kuwa, tangazo rasmi juu ya swala hili itatolewa hivi karibuni.

Wakala wa mwanadada huyu ameweka wazi tu kuwa ni kweli Lupita amekwishafuatwa na waongoza filamu wakumbwa mbalimbali kwaajili ya ofa ya kushiriki katika kazi zao huku akiacha swala la filamu ipi atashiriki kuwa ni fumbo.