Monday , 5th Dec , 2016

Kilele cha maonyesho ya mitindo ya mavazi 'Swahili Fashion Week' chafanyika jijini Dar es salaam, ambapo wanamitindo kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika walipata fursa ya kuonyesha ubunifu wao, pamoja na kutolewa tuzo kwa baadhi ya washiriki.

Kwenye tukio hilo lililofanyika usiku wa tar 4 Desemba 2016, mbunifu wa mavazi kutoka Tanzania Martin Kadinda aliibuka mbunifu bora wa mwaka wa mavazi ya kume, huku muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) akijinyakulia tuzo ya mtu maarufu kwenye mitindo (Most stylish icon).

Sambamba na hayo tukio lililoibua hisia kubwa ni pale Balozi Zakia Meghji aliponyanyuliwa kwenda kutoa tuzo ya 'Life achievement', ambayo ilikwenda kwa mwandishi na mpiga picha maarufu hapa nchini, Muhidi Issa Michuzi.

Watu wengine walioshinda tuzo ni Emanuel Kisusi (mwanamitindo bora wa kiume) , Jihan Dimach (Mwanamitindo bora wa kike), Waiswa Ronald (Mwanamitindo bora wa kiume Afrika Mashariki) Laduma Hhosa kutoka Afrika Kusini (Mbunifu bora wa mwaka Afrika).