Wednesday , 27th May , 2015

Msanii wa muziki Linex Sunday Mjeda, amesema kuwa amebadilisha mfumo wake wa maisha kwa kiasi kikubwa na amekuwa ni mtu wa kutokuonekana ovyo kutokana na kuziidisha kasi katika shoo, studio na kutafuta dili zitakazomuingizia kipato.

Linex

Linex ameeleza kuwa, katika nyakati hizi za sasa ni ngumu sana kumuona katika maeneo kama bar, akiwa muda mwingi anatumia katika maofisi na nyumbani akiwa anapumzika kutokana na ratiba yake kubana sana.

Kauli hii ya Linex ni kufuatia hisia alizokanusha vikali kuwa amepotea katika gemu sanaa yake haifanyi vizuri kama kipindi cha nyuma.