
Rais wa TFF Jamal Malinzi
Malinzi amefichua siri hiyo alipokua akitoa maelezo ya mfumo wa uendeshaji pamoja na mipango ya soka iliyo chini ya TFF katika kipindi hiki ambacho bado ni rais, wakati wa ziara ya waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye.
Hata hivyo pamoja na uwepo wa mipango hiyo mizuri ya timu za taifa za vijana ambazo zitakiimarisha kikosi cha taifa Stars, waziri Nape wamshauri Rais Wa TFF kuhakikisha anafanya ukaguzi wa fedha ili kukidhi haja ya kupata misaada ya kusogeza mbele maendeleo ya timu za taifa.
Katika hatua nyingine Waziri mwenye dhamana ya michezo Nape Nnauye amekemea tabia ya viongozi wa klabu kuacha malumbano na TFF pale wanapopewa maagizo fulani jambo ambalo lilijitokeza siku za hivi karibuni kwa viongozi wa Yanga.
Waziri Nape hii leo alizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea ofisi za shirikisho la soka nchini TFF kwa lengo la kujionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na taasisi hiyo kubwa ya soka hapa nchini