
Akiongea kwenye moja ya vipindi vya televisheni nchini Marekani, mke wa mchezaji huyo ambaye pia ni mwanamitindo na nyota wa televisheni Khloe Kardashian. amesema Lamar bado ana safari ndefu kwani hakumbuki vitu vingi.
"Ana safari ndefu, anajifunza jinsi ya kutembea na kula mwenyewe, kuunganisha maneno na mengineyo, ni hatua ndefu bado", alisema Khloe.
Khloe aliendelea kwa kusema kuwa Lamar hajui hata kile kilichomtokea na wanahofia iwapo watamuambia, inaweza ikamuathiri zaidi.
"Siwezi kumwambia, tunamwambia tu ameumia kwenye ubongo, lakini tumemwambia ameumiaje, kwa sababu itamrudisha kwenye hali yake, hajawahi kuuliza kwa nini yuko hapa", alisema Khloe.
Taarifa zaidi zinasema mchezaji huyo hana uwezo wa kutambua rafiki zake wa karibu na familia na kuwafanya madaktari kuwa na wasiwasi juu yake.
Lamar alipatwa na matatizo ya kiafya takriban mwezi sasa baada ya kukutwa amepoteza fahamu baada ya kuzidisha matumizi ya madawa huko Nevada Los Angels na kukimbizwa hospitali.