Saturday , 3rd Jan , 2015

Producer wa muziki kutoka studio ya Fishcrab ameeleza kuwa, project ya refix ya kazi za wasanii ambayo amekuwa akifanya kwa muda sasa, amejipanga kuikuza na kuwa anafanya matukio makubwa zaidi.

Lamar

Producer Lamar amesema kuwa atakuwa anazicheza na kuzi-dj mwenyewe na kuitambulisha Bongo Flava katika ulimwengu wa muziki wa Electro House.

Lamar amesema kuwa ataendelea kufanya refix hizi kutokana na aina ya muziki huo kuwa ndio unaofanya vizuri duniani, ukiwa umempatia pia sauti na muelekeo wake kama mtayarishaji muziki.