Wednesday , 30th Apr , 2014

Wakati tunaelekea katika tukio la kutuza wasanii wa muziki waliofanya vizuri kwa mwaka huu kupitia Kilimanjaro Music Awards 2014, zoezi la kuwapigia kura washiriki kukamilisha zile asilimia 70 za kuamua washindi, litafikia kikomo leo saa 6 usiku.

KTMA 2014

KIkiwa ni saa kadhaa tu zimebakia kuelekea kufikia kikomo cha zoezi la mashabiki kupiga kura, wito umetolewa kwa wote, mimi wewe na yule, kushiriki kupiga kura kwa wingi ili kumuwezesha msanii ambaye unaona anastahili tuzo hizo zenye kuheshimika mno Tanzania.

Zoezi hili limedumu kwa mwezi mzima, na ili kushiriki kupiga kwa njia ya sms andika namba ya mshiriki unayempenda na utume kwenda namba 15440 ama piga kura kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya https://www.kililager.com/ktma, kumbuka hujachelewa kupiga kura wahi sasa kabla ya saa sita usiku.