Msanii Chid Benz
Chid amefunguka hayo katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kwamba kwa sasa yupo vyema kuendeleza kazi nzuri za sana ya muziki kama alivyokuwa akifanya awali.
‘’ 'Kuna muda nafikiria nilikosa smile, nilikosa furaha ila sasa naona niko fresh, mambo mapya, stori mpya'' Amesema Chid
Aidha Chid Benz ameweka wazi kuwa kutokana na kujitoa kwa meneja wa Diamond Babu tale katika kuhakikisha kwamba anarejea sawa yeye ndiye atasimamia kazi zake pamoja na kwamba yeye hayupo chini ya ‘label’ ya WCB.
‘’Mimi nipo La Familia ila kazi zangu atasimamia Babu Tale na hili halina mgogoro wala tatizo lolote katika utendaji wa kazi’’ Amesema Chid Benz.
Aidha Chid Benz amewataka mashabiki kuendelea kufuatilia kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Chuma’ ambayo imetoka na nyingine ambazo nzuri zitatoka muda si mrefu.






