Friday , 2nd Oct , 2015

Msanii wa muziki wa nchini Kenya, Rufftone amekabidhiwa rasmi barua ya uthibitisho kama Balozi wa Mahusiano Mema kati ya Korea Kusini na nchi ya Kenya, akitajwa kupatiwa nafasi hiyo kutokana na mchango wake mkubwa kubadilisha maisha ya vijana.

Msanii wa muziki wa nchini Kenya Rufftone

Mratibu wa shughuli za ubalozi wa Korea Kusini nchini Kenya, Ki-Jun ambaye ndiye aliyemkabidhi Ringtone barua hiyo, amesema kuwa wana imani kuwa msanii huyo ataendelea kufanya kazi nzuri, kati ya majukumu yake ikiwa ni kuelimisha watu juu ya utamaduni wa Korea.

Ruftone ambaye alikuwa katika nafasi hiyo kwa takriban mwaka mzima, amefafanua kuwa kipindi chote hicho alikuwa katika majaribio, na hatimaye sasa kufanikiwa kushika nafsi hiyo baada ya ubalozi wa Korea Kusini kuridhishwa na jitihada ambazo amekuwa akizionyesha.