Monday , 14th Sep , 2015

Baada ya kudondoka rasmi Tanzania, Rapa K.O. kutoka Afrika Kusini atoa tathmini yake juu ya game ya muziki hapa nchini sambamba na kueleza wakali wa fani hiyo ambao anawahusudu kutoka hapa nchini.

Rapa K.O kutoka Afrika Kusini akiwa katika mahojiano na crew ya EATV

K.O katika maelezo yake, amemtaja msanii wa muziki Vanessa Mdee pamoja na msanii na mtayarishaji muziki Nahreel katika orodha yake hiyo, kama watu ambao pia amekwishafanya nao kazi na kuwaelewa na kukubali uwezo wao, ziara yake hii ikiwa ni kwaajili ya kukazia mpango huo.

K.O leo atasema mengi zaidi katika bonge moja la show, The Cruize ya East Africa Radio kuanzia saa 1 jioni, ambapo eNewz tutakuwa tukifuatilia mpango mzima na kukujuza kila Habari kuhusiana na tukio hilo.