Tuesday , 12th Aug , 2014

Nyota wa miondoko ya RnB/Pop na Afro-Beat nchini Rwanda- Kigali, James Ruhumuriza a.k.a King James yupo mbioni kufanya uzinduzi wa albam zake mbili baadae mwaka huu.

msanii wa nchini Rwanda King James

Mkali huyo ambaye anatambulika kwa kufanya muziki wake live jukwaani atakuwa ana jumla ya idadi za albam Sita huku akijiandaa kufanya uzinduzi huo mkubwa nchini humo.

Nyota huyo amekuwa akisafiri na kuhudhuria matamasha makubwa ya muziki kimataifa huku akijijengea jina kwa kufanya kazi na wanamuziki mbalimbali wa kimataifa.