Wednesday , 15th Apr , 2015

Rapa Young Killer, akiwa sehemu ya kundi kubwa la vijana ambao miaka 5 iliyopita hawakuwa na umri unaowaruhusu kisheria kupiga kura, baada ya kufikia umri huo ndani ya kipindi hiki, amewataka vijana wenzake kupiga kura mwishoni mwa mwaka.

Msanii wa miondoko ya bongofleva Young Killer

Young Killer amesema hayo kuunga mkono kampeni ya Zamu Yako 2015, kuhamasisha vijana kupiga kura, ambapo amesema kuwa, mwaka huu ni muda muafaka ambao umri na uelewa wao unaruhusu kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.