Saturday , 7th Jun , 2014

Timu nzima ya Kili Music Tour 2014, tayari imekwisha dondosha kikosi kizima pale Kahama tayari kwa ajili ya kudondosha bonge moja la burudani leo hii kwa wakazi wa mji wa kahama na vitongoji vyake pale katika uwanja wa Halmashauri.

Jukwaa la Kili Music Tour Kahama

Kama ilivyo ada ya ziara hii ya muziki ya Kili itawakutanisha wakazi wa Kahama na mastaa wakali watakaowasha moto jukwaani kama vile Shilole, Christian Bella, Madee, MwanaFA, AY, Rich Mavocal, Jambo Squad pamoja na Weusi.

Timu nzima ya EATV/ East Africa Radio tayari imekwisha shusha majeshi Kahama, hapa Zembwela, pale Mjukuu wa Ambua a.k.a Dullah na kwenye Mashine Dj Mackay kwa ajili ya kukuendeshea mpango mzima.

Itakuwa ni bonge moja la show, pale katika uwanja wa Halmashauri kuanzia saa 10 jioni, kwa kiingilio cha shilingi 2500 tu na kama hiyo haitoshi utapata zawadi ya bia moja ya Kilimanjaro Buree, Misosi pia itakuwepo.

Kili Music Tour 2014, Zungusha Kikwetu kwetu.