Saturday , 30th Aug , 2014

Siku ya leo jiji la Tanga linatarajiwa kuzizima na burudani kali za tamasha la Kili Music Tour, kwa onesho kubwa la mastaa wa muziki Bongo litakalofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga ambapo milango tayari imekwishafunguliwa kuanzia mida hii .

DJ Mackay Tayari kwa Stage ya Kili Music Tour Tanga, akiweka mitambo sawa sawa

Kwenye orodha ya mashambulizi, Jukwaa litakuwa na kazi ya kuhimili mikiki ya wasanii Ommy Dimpoz, Ben Pol, Weusi, Rich Mavocal, Khadija Kopa, Mzee Yusuph pamoja na Proffesa Jay.

Kikosi kizima cha East Africa Radio na East Africa Television kikiongozwa na Mjukuu wa Ambua, Zembwela aka Sniper na DJ Mackay wataamsha amsha katika burudani hii.

Burudani yote hii inaletwa kwako kwa kiingilio cha shilingi 3000 tu ambapo pia utapata kinywaji chako kimoja mlangoni bure.

Kilimanjaro Music Tour 2014, Zungusha Kikwetukwetu.