Friday , 4th Jul , 2014

Mwanamuziki nyota wa Burundi mwenye makazi yake nchini Kenya, Kidum amembatiza jina mnyama aina ya sokwe jina lake la utani akimwita sokwe huyo 'Kibido'.

Mwanamuziki wa Burundi Kidum

Kidum na msanii maarufu Jay Polly wa Rwanda alijumuika na wakazi wa eneo la Musanze nchini Rwanda katika onesho moja la muziki kutumbuiza katika sherehe zinazojulikana kama "10th Anniversary of Kwita Izina" (Gorillas naming) zilizofanyika huko Kinigi, katika jimbo la Musanze.

Sherehe hizo ziliendeshwa na mchekeshaji maarufu wa Rwanda Diogene Ntarintwa aka ‘Atom’ na kuhudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu Pierre Damien Habumuremyi.