Friday , 30th Jan , 2015

Msanii Eddy Kenzo wa Uganda, ameendelea kuweka nguvu nyingi katika sanaa yake mwanzoni kabisa mwa mwaka, akiwaleta pamoja mastaa wakubwa wa muziki Nigeria, Kcee, Wizkid pamoja na Limpopo katika kufanya video ya remix ya wimbo wake wa Jambole.

Msanii wa muziki nchini Uganda Eddy Kenzo

Staa huyu ambaye ameonesha dhahiri kutokutaka kupoteza nafasi ambazo amepata kuuvusha muziki wake, akiwa amepata nafasi ya kukutana na Akon pia nchini Gabon hivi karibuni, kabla ya kurejea Nigeria kukamilisha rekodi kadhaa akiwa anatarajia kukamilisha ziara yake hii kubwa kabisa na kurejea Uganda siku ya leo.

Kutokana na mafanikio ya kazi yake na jitihada anazoonesha, tayari Kenzo amejitengenezea utambulisho mzuri ambapo jarida maarufu huko Uingereza limemuingiza katika orodha ya wasanii wakali watano ambao wanaweza kufanya mambo makubwa kwa mwaka 2015.