Monday , 9th Feb , 2015

Star wa vichekesho wa nchini Uganda, Anne Kansiime ameeleza mapenzi yake makubwa kwa watoto huku akiwa na mpango wa kuanza kujenga familia kwa kuwa mama hivi karibuni.

Mchekeshaji nyota wa nchini Uganda, Anne Kansiime

Star huyu katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni amesema kuwa, mapenzi yake haya kwa watoto pia yamekuwa ni sababu kubwa kwa yeye kuigiza kama mtoto katika baadhi ya vichekesho ambavyo amekuwa akivifanya.

Kansiime ambaye ana umri wa miaka 27 sasa, ameweka wazi pia kuwa anapenda kuwa na watoto wengi bila kutaja idadi kamili huku akiwa na mpango wa kuanza kukuza familia yake hii kabla ya kutimiza miaka 30.