Monday , 1st Jun , 2015

Mchekeshaji Anne Kansiime wa nchini Uganda, amelaumu waandaaji wa show yake huko Afrika Kusini, kutokana na maandalizi mabovu ya onesho lake katika sherehe za tuzo za Star QT.

Mchekeshaji Anne Kansiime wa nchini Uganda

Kansiime ametoa baadhi ya kero zake kutokana na adha hiyo kuwa ni mitambo mibovu ya sauti na mipangilio mingine ambayo imemfanya kufanya onesho bovu kabisa.

Kansiime ammbaye alifika eneo la tukio kwa kuchelewa, lawama zake zikiende kwa promota wake kwa hilo pia, amesema kuwa atakubali kurudia tena kufanya onesho kwa mashabiki wake nchini humo, akiamini kuwa waandaaji watajipanga vizuri zaidi wakati ujao.

Onesho hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki hii pia likiwa kero kwa mashabiki waliohudhuria, ambapo wamelalamikia kiasi kikubwa cha pesa walicholipa na mwisho wa siku kushuhudia majaribio ya sauti wakati onesho limeanza tayari, na huduma na burudani ya kiwango cha chini.