Friday , 5th Jun , 2015

Mtayarishaji video anayeshikilia rekodi ya kushinda tuzo mbili za TAFA 2015, John Kallaghe amefunguka juu ya sababu za kuacha kufanya video za muziki, kubwa ikiwa ni mabadiliko ya soko na kupungua kwa wawezeshaji katika soko hilo.

John Kallage

Kallaghe ameiambia eNewz kuwa soko la utayarishaji video linabadilika kwa kasi kinguvu kazi na kiteknolojia likihitaji vipaji vipya na mtu aliye tayari kwenda kwa kasi hiyo, pili ikiwa ni kuanza kupotea kwa wadau ambao huwasimamia wasanii kufanya video.

Kallaghe ameeleza kuwa, kwa uzoefu wake wa kazi ya utayarishaji video, ni busara pia wakati mwingine kubadilika ili kutoa nafasi kwa vipaji vipya kuonesha uwezo, hatua ambayo inasaidia pia kuepusha ugomvi na pia kugombania wateja kama inavyoonekana kwa watayarishaji video wa sasa.