Wednesday , 27th Jan , 2016

Licha ya kueleza kuwa na rekodi za pamoja kati ya kapoz moto kabisa kutoka kiwanda cha Bongo Fleva, Jux pamoja na Vanessa, mastaa hao wameeleza kuwa licha ya kufanya pamoja kazi zaidi ya 6, hakuna mpango wowote kati yao wa kufanya albam ama EP.

Jux

Jux akiongea kwa niaba ya Vanessa, amesema kuwa upo mpango wa kuachia kolabo ya pamoja ikiwezekana baadaye mwaka huu, lakini kwa upande wa albam hawajafikiria wakizingatia ukubwa wa hatua hiyo na mazingira halisi.

Pembeni ya suala hilo, tukataka kufahamu kidogo juu ya ratiba ya Jux ambaye hivi karibuni alirejea shule huko China kuendelea na masomo, wiki 5 baadaye akatua tena nchini, ambapo amesema kuwa, kilichomrudisha mapema nchini ni likizo na pia mpenzi wake - Vanessa Mdee.

Tags: