Saturday , 8th Mar , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo, Juma Jux baada ya kuukataa ukweli kwa muda mrefu sasa, hatimaye baada ya kuachia ngoma yake mpya ya Nitasubiri, Leo hii amekiri ukweli kuwa ngoma hii kwa namna mo

Jux amesema haya leo katika mahojiano aliyofanya katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, wakati akizungumzia kuhusiana na wazo lililomsukuma kuandika ngoma ya namna hii ambayo katika mahojiano yake ya awali na eNewz, alisema kuwa kazi hii inatokana na hisia za ukweli japokuwa haikuwa inamhusu Jackie.

Kauli hii mpya ya Jux inaendelea kuthibitisha ukweli juu ya kuwepo kwa mahusiano ya kimapenzi kati yake na Jackie ambaye mpaka sasa anaaminika kuwa yupo kizuizini huko China ingawa msanii huyu binasfi amesema kuwa, yeye na Jackie ni Marafiki tu na ana mpenzi wake ambaye hayupo tayari kumuweka wazi.