Tuesday , 23rd Sep , 2014

Julio Batalia, msanii wa Bongofleva nchini amewataka wasanii wa Tanzania kuongeza upendo ushirikiano na umoja ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi nzuri zaidi na kufanya muziki wa Tanzania utambulike vizuri Afrika.

msanii wa bongofleva nchini Julio Batalia

Julio amesema haya sambamba na kutangaza ujio wa zawadi kwa mashabiki wake, ngoma ya Special for You ambayo ameifanya pamoja na swahiba wake, Chegge Chigunda ambayo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji.