Sunday , 20th Jul , 2014

Mwanamuziki nyota wa kike wa nchini Uganda Juliana Kanyomozi amefiwa na mtoto wake wa kiume huko jijini Nairobi nchini Kenya.

Mwanamuziki wa Uganda Juliana Kanyomozi

Vyanzo vya habari habari kutoka nchini Uganda na Jijini Nairobi vimeelezea kuwa mtoto wake huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 11 anayeitwa Keron, amefariki katika hospitali Aga Khan iliyopo Jijini Nairobi.

Imeelezwa kuwa mtoto wa mwanamuzki huyo alipatwa na ugonjwa wa pumu akiwa shuleni. eNewz inatoa pole kwa Juliana Kanyomozi kwa msiba huu mzito.