Wednesday , 2nd Dec , 2015

Rapa Jua Cali kutoka nchini Kenya, amesema kuwa kwa upande wa muziki wake anafanya mchakato kwa ajili ya kufanyakazi na mtayarishaji muziki wa kimataifa, Dr Dre.

Jua Cali amesema kuwa, endapo mpango huo utakamilika, utasaidia kwa kiasi kikubwa kuiweka sanaa yake katika ramani ya kimataifa, akiwa pia na albam ambayo inasimama kwa jina Mali ya Uma njiani, kazi ambayo ilitakiwa kutoka mwezi Septemba kabla ya kusogezwa mbele.

Endapo rapa huyo atafanikisha mipango hiyo, ataweka rekodi ya kuwa rapa wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kufanya kazi na Dr Dre, ambaye mbali na kubeba heshima ya kutengeneza misingi ya muziki wa Hip Hop, anabakia kuwa mtayarishaji muziki bora wa wakati wote wa muziki huo tangu miaka ya 90.